Rais Xi Jinping wa China ameendesha mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na kusikiliza ripoti kuhusu mwitikio wa ajali ya ndege ya China Eastern iliyotokea hivi karibuni.
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo Rais Xi alitoa amri kuanza uchunguzi mara moja, kazi ya utafutaji na uokoaji, hatua za baada ya ajali hiyo, na kutafuta chanzo cha ajali hiyo, kuwafariji wanafamilia wa wahanga na kuwapatia msaada.
Imefahamika kwenye mkutano kuwa idara husika zilianza mara moja kutekeleza maagizo, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya usafiri wa anga na ya uokoaji wa dharura.
Pia mkutano huo umesema kazi zilizobaki ikiwa ni pamoja na kutambua na kurudisha mabaki ya wahanga, inatakiwa kufanyika vizuri. Vile vile habari husika zinatakiwa kutolewa kwa wakati, kwa usahihi, na kwa uwazi ili kujibu ufuatiliaji wa watu.