Nenda kwa yaliyomo

Violeta Parra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Violeta Parra
Violeta Parra katika miaka ya 1960s.
Violeta Parra katika miaka ya 1960s.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Violeta Parra del Carmen Sandoval
Amezaliwa 4 Oktoba 1917
Asili yake San Carlos,Chile
Amekufa 5 Februari 1967
Aina ya muziki Nyimbo za Kilatini
Kazi yake Mwanamuziki,Mwanasiasa,Msanii
Miaka ya kazi 1949-1965
Studio EMI-Odeon
Alerce
Warner Music
Tovuti Tovuti Rasmi


Historia

[hariri | hariri chanzo]

Violeta Parra del Carmen Sandoval (4 Oktoba 1917 - 5 Februari 1967) alikuwa mwanamke mashuhuri na maarufu wa Chile .Alikuwa msanii wa hadithi na wa vitu vya kuonwa. Yeye ndiye aliyeweka msingi wa "New Song," La Nueva Cancion chilena, mtindo mpya na bora wa kuimba hadithi za Kichile.Mtindo huu ungesambaa na kuenea huku ikishawishi watu wengine bali na Wachile tu.

Parra alizaliwa katika eneo la San Carlos,katika mkoa wa Ñuble, mji mdogo uliokuwa kusini mwa Chile. Alikuwa mhusika katika harakati za maendeleo za Chama cha Socialist Party cha Chile. Yeye ndiye aliyerudisha Peña(inayojulikana sasa kama La Peña de Los Parra). Peña ni kituo cha jamii cha sanaa na harakati za kisiasa za kupinga dhuluma kwa raia. Baadhi ya watu hufikiri yeye ndiye aliyeanzisha Peña ya kwanza lakini katika rekodi za Shule ya Kifalme ya Lugha ya Kihispania,pahala kama hizi ziliitwa hivyo tangu mwaka wa 1936. Wakati wa serikali ya Rais Salvador Allende kulikuwa na maPeña kote nchini Chile. Hivyo basi zikapigwa marufuku na serikali ya kijeshi iliyotoa Allende na wenzake. Serikali mpya ikafanya wafungwa na wakimbizi wengi kutoka sekta za sanaa na masomo ya Chile. Hata hivyo, bado kuna maPeña mengi yanayoendelea kote Chile,America,[[Amerika ya Kaskazini],Uropa na Australia. Watu katika maPeña haya wanaendelea kuerevusha na kusomesha jamii ya Wachile waliotoroka Chile baada ya mapinduzi ya kijeshi ya 11 Septemba 1973 iliyomtoa Rais Salvador Allende.

Violeta Parra alikuwa mmoja wa familia mashuhuri ya Parra. Kaka yake alikuwa mshairi mashuhuri wa kisasa, anafahamika zaidi kama "anti-mshairi", Nicanor Parra. Mwanawe, Angel Parra, na binti yake, Isabel Parra, walikuwa pia watu muhimu katika maendeleo ya Nueva Canción Chilena. Watoto wao ,pia, wamejihusisha na mila ya sanaa katika familia yao.

Violeta Parra alijiua kwa kujipiga risasi kwa kichwa katika mwaka wa 1967 kwa sababu ya huzuni kwa kuvunjika kwa uhusiano wake na Gilbert Favre.

Kaburi ya Violeta Parra

Wimbo wake unaojulikana zaidi ni Gracias a la Vida(Asante kwa maisha), iliyopigiwa debe Amerika ya Kusini na Mercedes Sosa na hapo baadaye Marekani na Joan Baez. Huu ndio mmojawapo wa nyimbo zinazojulikana kabisa katika Amerika ya Kilatini katika historia.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za Studio

[hariri | hariri chanzo]
  • Chants et danses du chili. Vol. 1 (1956)
  • Chants et danses du chili. Vol. 2 (1956)
  • Violeta Parra, Canto y guitarra. El Folklore de Chile, Vol. I (1956)
  • Violeta Parra, acompañada de guitarra. El Folklore de Chile, Vol. II (1958)
  • La cueca presentada por Violeta Parra: El Folklore de Chile, Vol. III. (1958)
  • La tonada presentada por Violeta Parra: El Folklore de Chile, Vol. IV. (1958)
  • Toda Violeta Parra: El Folklore de Chile, Vol. VIII (1960)
  • Violeta Parra, guitare et chant: Chants et danses du Chili. (1963)
  • Recordandeo a Chile (Una Chilena en París). (1965)
  • Carpa de la Reina (1966)
  • Las últimas composiciones de Violeta Parra (1967)

Diskografia ya baada ya kifo

[hariri | hariri chanzo]
  • Violeta Parra y sus canciones reencontradas en París (1971)
  • Canciones de Violeta Parra (1971)
  • Le Chili de Violeta Parra (1974)
  • Un río de sangre (1975)
  • Presente / Ausente (1975)
  • Décimas (1976)
  • Chants & rythmes du Chili (1991)
  • El hombre con su razón (1992)
  • Décimas y Centésimas (1993)
  • El folklore y la pasión (1994)
  • Haciendo Historia: La jardinera y su canto (1997)
  • Violeta Parra: Antología (1998)
  • Canciones reencontradas en París (1999)
  • Composiciones para guitarra (1999)
  • Violeta Parra - En Ginebra, En Vivo, 1965 (1999)
  • Violeta Parra: Cantos Campesinos (1999)

Masomo zaidi

[hariri | hariri chanzo]
  • Moreno, Albrecht: "Violeta Parra and 'La Nueva Canción Chilena.'" Kitabu kuhusu tamaduni mbalimbali za Amerika ya Kilatini 5 (1986): 108—26.
  1. ^ Mena, Rosario. "Eduardo Parra: My Sister Violetta Parra". http://www.nuestro.cl/eng/stories/profiles/lalo_parra.htm Archived 29 Oktoba 2009 at the Wayback Machine..

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]