Ugali
Ugali ni chakula kinacholiwa na jamii za kiafrika. Chakula hiki chenye virutubisho vya wanga hutokana na unga wa nafaka (kama mahindi, mtama, uwele) au muhogo.
Ugali hutayarishwa kwa njia ifuatayo: kwanza unachemsha maji kwenye sufuria baada ya kuchemka unachanganya unga kidogo na maji ya baridi pembeni, kisha tia mchanganyiko huo kwenye maji ya moto yaliyo jikoni huku ukikoroga. Utatokea mchanganyiko wa unga na maji ambao unaitwa uji, acha uji huo uchemke kwa muda kisha tia unga kiasi kulingana na uji wako huku ukisonga kwa kutumia mwiko. Endelea kusonga mpaka mchanganyiko ushikamane, mchanganyiko huu ndio hutoa ugali.
Kimaeneo kuna aina mbalimbali za ugali kutegemeana na aina za mazao yanayopatikana.
- Udaga ni ugali unaopikwa kwa kuchanganya unga wa muhogo na ulezi, hupatikana zaidi maeneo ya Musoma kwa Wakuria
Ugali huweza kuliwa na mboga ya aina yoyote kama vile mboga majani, sukumawiki, samaki na nyama.
Kawaida ugali huliwa kwa mikono mitupu. Tonge la ugali hufinyangwa kwa mkono kisha kuchovya kwenye maziwa au mchuzi wa maharage, samaki, au nyama ya ng'ombe. Ugali, mapishi yake na jinsi unavyoliwa, hufanana kwa kiasi fulani na foufou toka Afrika Magharibi, na polenta toka Italia. Ugali hujulikana kama nshima nchini Zambia au nsima nchini Malawi.
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ugali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |