The Rolling Stones
The Rolling Stones ni bendi ya muziki aina ya rock and roll kutoka Uingereza iliyoanzishwa mwaka 1962. Iliundwa na Mick Jagger (mwimbaji), Keith Richards (gitaa), Brian Jones (gitaa), Bill Wyman (besi) na Charlie Watts (ngoma).
Mwanzoni walijaribu kuiga blues na rock and roll ya Marekani kwa mfano wanamuziki kama Chuck Berry na Muddy Waters lakini baadaye waliendelea kuunda staili yao.
Walipendwa sana na vijana duniani wakishindana na kundi la The Beatles.
Walifaulu mara ya kwanza 1965 kwa wimbo "The Last Time" na "(I Can't Get No) Satisfaction". Yaliyofuata ni pamoja na "Paint It Black", "Sympathy for the Devil" na "Jumpin' Jack Flash" (1968).
Brian Jones aliondoka katika kundi 1969 akifuatwa na Mick Taylor aliyeshiriki katika nyimbo kama "Brown Sugar", "Tumbling Dice" na "Angie" akaondoka 1974. Baadaye Ron Wood alijiunga na kundi.
Hata kama wamezeeka pamoja Rolling Stones wameendelea kucheza hadi leo.
Albumu kadhaa
[hariri | hariri chanzo]- The Rolling Stones (1964)
- The Rolling Stones No. 2 (1965)
- Out of Our Heads (1965)
- Aftermath (1966)
- Between the Buttons (1967)
- Their Satanic Majesties Request (1967)
- Beggars Banquet (1968)
- Let It Bleed (1969)
- Sticky Fingers (1971)
- Exile on Main St. (1972)
- Goats Head Soup (1973)
- It's Only Rock 'n Roll (1974)
- Black and Blue (1976)
- Some Girls (1978)
- Emotional Rescue (1980)
- Tattoo You (1981)
- Undercover (1983)
- Dirty Work (1986)
- Steel Wheels (1989)
- Voodoo Lounge (1994)
- Bridges to Babylon (1997)
- A Bigger Bang (2005)
- Blue & Lonesome (2016)
- Hackney Diamonds (2023)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu The Rolling Stones kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |