Nenda kwa yaliyomo

Yai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mayai)
Mayai ya ndege na samaki mbalimbali

Yai ni njia ya wanyama jinsi wanavyozaa kama vile ndege, reptilia, samaki na wadudu wengi. Mayai ya mamalia na wanyama wengine kadhaa hukua ndani ya mwili, katika uterasi kwa kawaida.

Ni seli ambayo hutokana na kiumbe jike, ikiungana na seli ya dume ni chanzo cha kiumbe kipya au mtoto. Kwa wanayama kama mamalia wengi seli hii inaweza kubaki ndani ya mwili na kuendelea humo.

Kwa lugha ya kawaida ni seli ile ya chanzo pamoja na akiba ya lishe kwa ajili ya kipindi cha kwanza katika maisha ya kiumbe kipya inayotegwa na mnyama nje ya mwili ili kiumbe kipya au mtoto aendelee huko hadi pindi atakapo kuwa yuko tayari kutoka kwenye yai. Mayai huwa na ganda ya kulinda maisha mapya ya kiumbe ndani yake.

Kutokana na kiwango cha proteini, mafuta na vitamini ya lishe ndani yake, mayai hutafutwa kama chakula na wanyama na pia na binadamu.

Wikimedia Commons ina media kuhusu: