Alka (kutoka Kiiceland: alka) ni ndege wa bahari wa familiaAlcidae. Wanafanana na ngwini kwa sababu wana umbo na rangi sawa na hawa, pia mabawa mafupi lakini spishi ziliopo hadi sasa zinaweza kuruka angani kinyume na ngwini. Spishi nyingine zilozokwisha sasa zilikuwa zimepoteza uwezo kuruka angani (k.m. Great Auk). Wanatokea bahari za nusudunia ya kaskazini. Huzamia kabisa ili kukamata samaki, gegereka na krili. Huzaa katika makoloni kwa pwani zenye miamba. Jike hulitaga yai moja tu juu ya shubaka la mwamba au katika tundu.
Makala hii kuhusu "Alka" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili alka kutoka lugha ya Kiiceland. Neno (au maneno) la jaribio ni alka. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.