Nenda kwa yaliyomo

Mwanzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Karibu kwenye Wikipedia,
Hadi leo tuna makala takriban 96,360 kwa Kiswahili

Je unapenda kuona Wikipedia yetu kama kitabu? Bofya hapa!
     

     

Kamusi Elezo ya Kiswahili

Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!

Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.

Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.


Je, wajua...

Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:

Ngorongoro

  • ... kwamba Hifadhi ya Ngorongoro imepokewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO?
  • ... kwamba Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
  • ... kwamba Septemba 1752 ilikosa siku kumi na moja? Katika Dola la Uingereza, ulikuwa mwaka pekee wenye siku 355, kwani Septemba 3-13 zilirukwa wakati Dola lilipopitisha kalenda ya Gregori.
  • ... kwamba Samia Hassan Suluhu ni rais wa kwanza mwanamke Afrika ya Mashariki? Aliapishwa kuwa rais mara baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Pombe Magufuli.


  • Makala ya wiki

    Ramadan au ramadhani, (kwa Kiarabu: رمضان) ni mwezi wa tisa katika Kalenda ya Kiislamu na mwezi wa kufunga katika Uislamu kuadhimisha ufunuo wa kwanza wa Qur'an kutona na mafundisho ya Mtume Muhammad. Mwezi huo huwa na siku 29 au 30 kutegemeana na kuonekana kwa mwezi.

    Kufunga ni moja ya Nguzo tano za Uislamu. Mwislamu mzima, mwenye afya nzuri, anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mchana kutwa, pamoja na kujizuia kufanya mapenzi toka alfajiri hadi magharibi.

    Matendo hayo ya toba yanaendana na kuswali sana na kusoma Quran kwa wingi.

    Kwa wagonjwa, wanaosafiri, wazee, wajawazito, wanaonyonyesha na wanawake wenye hedhi sio lazima kufunga.

    Mwisho wa Ramadhani ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Waislamu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kuswali, baadaye hukutana kwenye karamu.

    Neno Ramadhani linatokana na mizizi ya Kiarabu ramiḍa au ar-ramaḍ, ambayo inamaanisha joto kali au ukavu. ►Soma zaidi


    Picha nzuri ya wiki

    Samia Sulu Hassan

    Samia Suluhu Hassan ni rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha hii ni 2011 akiwa Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam.

    Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili

    • Idadi ya makala: 96,360
    • Idadi ya kurasa zote: 193,025 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
    • Idadi ya hariri: 1,399,965
    • Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: 74,249
    • Idadi ya wakabidhi: 15
    • Idadi ya watumiaji hai: 767 (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
    Bofya hapa kwa kupata namba za sasa
    Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
    Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
    (fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
    • na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
    (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)

    Michango ya wanawiki: angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia (andika jina la mtumiaji kwenye sanduku)

    Jumuia za Wikimedia

    Commons
    Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
    Meta-Wiki
    Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
    Wikamusi
    Kamusi na Tesauri
    Wikitabu
    Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
    Wikidondoo
    Mkusanyiko wa Nukuu Huria
    Wikichanzo (Wikisource)
    Matini za vyanzo asilia kwa Kiswahili
    Wikispishi
    Kamusi ya Spishi
    Wikichuo
    Jumuia ya elimu
    Wikihabari
    Habari Huru na Bure